Rais wa Zimbamwe, Robert Mugabe ameteuliwa na chama chake ZANU-PF kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2018

Kiongozi huyo ameanza kutawala nchi hiyo toka wapate uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Wakoloni wa Kingereza.

Baadhi ya makundi yameibuka huku yakipinga kiongozi huyo mwenye miaka 92 kuendelea kuliongoza taifa hilo kwa madai kuwa ameshusha uchumi wa nchi hiyo.

Mugabe anasifika kwa kuwa rais mwenye misimamo thabiti licha ya kuwa mzee, lakini akisimamia jambo na kuamua lifanyike lazima lifanyike na hata kama akikataa jambo anamaanisha amekataa haswa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *