Ukitaka kutumia kiki kwa kumtumia Mr. Blue jiulize ‘nahatarisha ndoa yake?’ kama hujajiuliza swali hilo ‘sahau kutumia jina la staa huyo’.

Staa huyo wa muda mrefu kwenye gemu ya Bongo Fleva ambaye ana heshima kubwa kutokana na historia yake ya muziki, Mr. Blue a.k.a Byser ametoa TAHADHARI, ONYO lakini pia unaweza ukaiita TANBIHI kwa wadau wote wa Bongo Fleva.

Blue ambaye mwezi uliopita alipamba vyombo vya habari kwa kashfa ya kudate na mpenzi wake wa zamia ambaye kwa sasa ni mpenzi wa wazi wa Barakah The Prince, Naj.

Taarifa zilizozagaa zikadai kuwa Mr. Blue ameandikwa kwa jina la kike kwenye simu ya Naj ili wawili hao watakapokuwa wanawasiliana watu wengine wasitambue, akiwemo Barakah.

Baada ya tetesi hizo kushika kasi, Blue akajitokeza na kuwatuhumu Barakah na Naj kwa kutumia jina lake kuipa kiki ngoma mpya wanayojipanga kuitoa lakini kama hiyo haitoshi akakanusha kuwasiliana na Naj kimapenzi.
Na akadai kuwa ‘ndoa yake’ imetetereshwa na tuhuma hizo kwakuwa siku zote amekuwa mwaminifu kwa familia yake.

Baada ya siku kadhaa Baraka The Prince nae akajitokeza na kudai ‘anapopataka Mr. Blue waelekee, basi wataenda hivyo hivyo’ kwakuwa yeye (Barakah) amemtunzia Blue heshima yake kwa kipindi chte hicho lakini kilichotokea kwa sasa hakikuwa kizuri. Kipi? Blue kurudiana na Naj kimya kimya? Au Blue Blue kudai jina lake linatumiwa kuwapa kiki Barakah na Naj?

Yote kwa yote Blue ametoa tahadhari mpya, atayehatarisha usalama na ustawi wa ndoa yake ‘ATAPAMBANA NAE MAHAKAMANI’ period!

Bayser ameamua kuweka tahadhari ambayo huenda mastaa na fans wa Bongo Fleva hawajaielewa vizuri au hawajui athari yake ‘kikazi’.

Kuhatarisha ndoa ya Blue ni pamoja na kushiriki kwenye video ukiwa na Blue kisha kufanya jambo ambalo familia yake itasema ‘ndoa basi’!!

Kuhatarisha ndoa ya Blue ni mwanamke kuwa mrembo sana hadi Blue achanganyikiwe kisha atake kukuoa na pindi mke wake anapokataa na kudai ndoa ivunjike huko ni kuhatarisha ndoa ya Blue.

Kuhatarisha ndoa ya Blue ni kufanya kazi na Blue hadi siku au nyakati ambazo familia yake itamuhitaji na ikatishia kuvunjika kwa ndoa yao iwapo hatorudi (licha ya kuwa ana mkataba wa kufanya kazi (na mtu/kampuni/taasisi fulani) kwa wakati huo.

Kuhatarisha ndoa ya Mr. Blue kuna tafsiri pan asana kwenye upande wa kisheria ingawa haitoshangaza kuona kuwa tafsiri kubwa inayopewa kipaumbele hapa ni ‘kudai unatembea na Blue au kudai Blue na Naj (mwanamke fulani wana uhusiano wa kimapenzi n.k

Kabla ya Blue kuiona tafsiri ya kauli hii kwa namna ndogo sana awaeleweshe wadau wake mipaka ya tafsiri ya kauli hii vinginevyo ‘atakosa dili za kazi kwa watu wanaozingatia haki za watu na kuheshimu kauli za watu kwa kadri zilivyozungumzwa na zinachomaanisha’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *