Serikali ya mkoa wa Mtwara imeendelea kupokea misaada kwa ajili ya kusaidia baadhi ya watanzania walioondolewa nchini Msumbiji kinyume na taratibu ili warudishwe makwao.

Akipokea msaada wa shilingi laki tano kutoka kwa meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mtwara, Mkuu wa mkoa huo Halima Dendego amesema kuwa idadi ya watanzania waliorudishwa kutoka Msumbiji imefikia 5634.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa kwasasa idadi ya watanzania wanaotoka Msumbiji imepungua tofauti na kipindi cha nyuma kutokana na wengi wao kurejea na kupelekwa makwao.

Pia Bi. Halima Dendego amesema kuwa msaada huo utamfikia Agnesi Charles aliyeachiwa mtoto wa mwaka mmoja na rafiki yake Jaquline Greyson ambaye alifariki dunia mara baada ya kuingia nchini akiwa mgonjwa.

Wiki chache zilizopita watanzania wamerudishwa kutoka Msumbiji kutokana na kuingia nchini humo bila vibali maalumu vya kuishi katika nchi hiyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *