Kituo cha MTV kimemtaja staa wa Marekani, Kanye West kushika namba moja ya wanamuziki wa hip hop waliofanya vizuri mwaka 2016 baada ya kuwakalisha wanamuziki wenzake nchini humo.

Nafasi ya pili imeshikwa na rapa Drake ambaye naye mwaka huu ulikuwa wake baada ya kufanya nyimbo kibao zilizompa kiki zaidi kwenye muziki huo nchini Marekani.

Vigezo vilivyosababisha Kanye West kushika namba moja kwenye orodha hiyo ya rapa bora Marekani ni mashairi, wingi wa mashabiki na kukubalika katika jamii.

Rapper huyo amewafunika wasanii wengine akiwemo Drake, Kendrick Lamar, Young Thudg na wengine.

Charlamagne amevitaja vigezo vilivyotumika kuwapata wasanii kumi wa Hip Hop waliofanya vizuri kwa mwaka huu ni pamoja na mashairi makali, ukubwa wa muziki wao kwa mashabiki, mitindo yao na uwepo wao kwenye jamii.

Orodha nzima ipo kama ifuatavyo.

1. Kanye West
2. Drake
3. Chance the Rapper
4. Travis Scott
5. Future
6. Young Thug
7. YG
8. Kendrick Lamar
9. Lil Uzi Vert
10. 21 Savage

MTV huwa na utaratibu wa kutoa orodha ya marapa bora waliofanya vizuri ndani ya mwaka husika kutokana na kazi za msanii kupokelewa vizuri ndani ya jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *