Wandaaji wa tuzo za MTV EMA wamempokonya Wizkid tuzo ya Best African Act na Worldwide Act na kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda tuzo hiyo.

Katika utoaji wa tuzo hizo staa wa Nigeria, Wizkid alitangazwa mshindi lakini kwenye website ya tuzo hizo kura zilikuwa zinaonesha Alikiba ndiye aliyeshinda katika kipengele hicho.

Kupitia ukarasa wake wa Facebook Alikiba amethibitisha taarifa hizo wakati akichat live siku ya jana na kuwaambia mashabiki wake.

Alikiba amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali wa tuzo hiyo na sio Wizkid kama ilivyodaiwa.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa habari hizo amezipokea kwa furaha kubwa na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kushinda na kuwa nyuma yake katika tuzo hizo.

Kwa upande wa Wizkid, tayari amefuta post zote za Instagram alizokuwa ameweka kushangilia ushindi wa tuzo hiyo.

Katika kipengele hicho Alikiba alikuwa akichuana na wasanii kama vile Black Coffee kutoka Afrika Kusini, Wizkid na Olamide kutoka Nigeria pamoja na Casper Nyovest kutoka Afrika Kusini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *