Mtoto wa aliyekuwa gwiji wa soka wa Brazil, Pele anayeitwa Edinho amejisalimisha kwa maafisa wa magereza kwenda kutumikia kifungo alichohukumiwa kuhusiana na makosa ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Edinho ambae alikuwa golikipa wa klabu ya Santos nchini humo alikuwa ameachiwa huru wakati rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 33 ilipokuwa ikisikizwa.

Lakini japo mahakama ya mjini Sao Paulo imeamua kupunguza kifungo hicho hadi miaka 12 imemtaka arudi gerezani wakati kesi ya rufaa aliyoiwasilisha ikiendelea kusikizwa.

Edinho kwa upande wake amekuwa akikana mashtaka hayo ya uzaaji wa dawa za kulenywa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *