Mtoto wa Muhammad Ali, Muhammad Ali Jnr amezuiliwa na kuhojiwa kwa saa mbili katika uwanja wa ndege wa Florida baada ya kuwasili kutoka Jamaica mapema mwezi huu kutokana na jina lake la Kiarabu.

Wakili wa familia ya Muhammd Ali Chris Mancini alinukuliwa akisema kuwa kuzuiliwa kwa Muhammad Ali Jnr kulihusishwa moja kwa moja na jaribio la rais Trump kuwapiga marufuku Waislamu kutoka mataifa saba ya Waislamu kuingia Marekani.

Kwa uapnde mwingine mcheza filamu mmoja kutoka Syria, Khaleed Khateeb ambaye alishiriki katika filamu ilioteuliwa kuwania tuzo za Oscar amezuiliwa kuelekea katika sherehe za tuzo hizo mjini Los Angeles.

Khaleed Khateeb alipewa Visa ya Marekani lakini akazuiliwa kupanda ndege iliokuwa ikielekea Marekani .

Kampuni hiyo ya ndege imesema kuwa maafisa wamepata habari mbaya kumuhusu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *