Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Lil Wyne juzi alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa hotelini akiwa hajitambui.

Baada ya kufanyiwa matibabu watu wa karibu wa rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 walitaka kumtoa hospitali ili aweze kufanya onyesho mjini Las Vegas lakini madaktari walimshauri Wyne apumzike na asipande ndege katika kipindi hiki.

Binti wa Lil Wyne ambaye ni mtoto wake wa kwanza Reginae Carter amewatoa hofu mashabiki duniani kote waliokuwa na wasi wasi juu ya maendeleo ya afya ya Lil Wayne baada ya kuandika ujumbe kwenye mtandao wa Tweeter unaoashiria hali ya baba yake kuwa nzuri.

”Baba yangu anaendelea vizuri nashukuru kwa kila aliyeguswa, usiamini kila unachokisikia” aliandika Reginae Carter.

Miaka minne iliyopita Lil Wyne alilazwa kwa siku kadhaa katika hospitali ya Los Angeles na baadae alikiambia kituo cha redio cha Power 106 kuwa amekuwa akisubuliwa na tatizo hilo la kupoteza fahamu mara kwa mara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *