Mtendaji wa Kiijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti, Shamte Rashidi Makawa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho nyumba yake imechomwa moto baada ya kuwatoroka wauaji hao wilani humo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi tayari lipo eneo la tukio, hivyo watatoa taarifa rasmi za tukio hilo baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *