Mtandao wa Jay Z, Tidal watangaza perfomance ya Alikiba London

0
602

Mtandao wa kuuza muziki wa TIDAL ambao upo chini ya rapa Jay Z umetangaza perfomance ya mwanamuziki kutoka Alikiba kwenye Tamasha lililofanyika jijini London nchini Uingereza.

Kupitia akaunti yao mtandao huo umeandia kuwa ‘The unstoppable AliKiba is live right now in London”.

Alikiba ni miongoni mwa wanamuziki kutoka Afrika walioshiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika mwisho wa wiki nchini Uingereza.

Tamasha hilo lilihusisha wasanii kama vile Cassper Nyovest, P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Tekno , MI.

Alikiba akitumbuiza kwente Tamasha hilo lililofanyika jijini London nchini Uingereza.
Alikiba akitumbuiza kwente Tamasha hilo lililofanyika jijini London nchini Uingereza.

Tanzania iliwakilshwa na Alikiba ambaye alipata nafasi ya kufanya ya kuimba nyimbo zake kama vile Mwana na Aje ambayo kwa mara ya kwanza amepata nafasi ya kuimba wimbo huo na M.I aliyemshirikisha.

Mashabiki wengi wameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Alikiba kushiriki katika tamasha hilo kubwa huku akiwa na wasanii wakubwa kibao, kwani wanaamini jambo hilo linazidi kumjenga na kufungua njia zaidi katika kazi yake hiyo ya muziki.

LEAVE A REPLY