Kampuni ya Ant Financial inayomiliki mtandao wa biashara wa Alibaba inatarajia kuinunua kampuni ya kimarekani ya MoneyGram kwa dola milioni 880.

MoneyGram ina karibu vituo 350,000 kwa karibu nchi 200 huku Ant Financial ikiwa na watumiaji milioni 630.

Kununuliwa kwa MoneyGram kutahitaji kudhinishwa na kamati ya Marekani ya masuala ya uwekezaji wa kigeni.

Eric Jing, ambaye ni mkurugeni mkuu wa Ant Financial, amesema kuwa kuunganishwa kwa kampuni hizo mbili kutawawezesha watu kote duniani kutuma pesa kwa njia rahisi, hasa katika mataifa makubwa kama marekani, China, India, Mexico na Ufilipino.

Ununuzi huo utaisaidia kumpuni hiyo kupanua huduma zake katika mataifa ya kigeni wakati inakabiliwa na ushindani kutoka kwa kampuni ya Tencent’s WeChat.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *