Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, madiwani na baadhi ya wananchi leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.
Kwa nyakati tofauti kuanzia Septemba 14 hadi 17 walikamatwa na polisi wakituhumiwa kuhusika kufunga barabara za kuingia kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).
Septemba 14 madiwani wa halmashauri mbili za Wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani zinazotokana na ushuru wa huduma.