Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma amemtaka Rais Magufuli kutosikiliza kelele za baadhi ya viongozi wa upinzani kuhusu utendaji kazi wake.

Msukuma alisema hayo wakati wa makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF).

Amesema wao Geita wapo mstari wambele kuhakikisha wanaunga mkono kila jambo ambalo linafanywa na Rais Magufuli.

Mbali na hilo Msukuma alikuwa na ombi kwa Rais Magufuli pindi wawekezaji waliokuwa wakisafirisha makinikia kwenda nje ya nchi wakilipa deni hilo basi awakumbuke watu wa Geita japo kwa barabara za lami kwani barabara zimekuwa hazina kiwango kizuri na ni mbovu.

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsifu sana mbunge msukuma na kusema hata bungeni huwa anamsikia anasimamia sana chama chake (CCM) na kusema kuwa yupo vizuri sana kwa jambo hilo, kwani anawakilisha vizuri sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *