Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma amesema kuwa Rais Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege ya Tanzania  Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema wapinzani wanatafuta kiki.

Mbunge Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali ilivyosema na kudai Rais Magufuli hausiki katika jambo hilo.

Aidha Mbunge huyo aliendelea kudai jumla ya deni la bilioni 87 ambayo serikali ya Tanzania inadaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kwa kuvunja mkataba wa kazi halijatokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli.

“Deni hili siyo kwamba limetokana na uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini kama Rais huwezi kukataa deni ambalo serikali inadaiwa akiwa madarakani lakini pia suala hili lipo mahakamani na hatua iliyofikia ni hatua ya mwanzo kabisaa, na si kweli kwamba ndege imekamatwa unaweza kuingia mitandaoni ukaiona ndege ilipo, bado ipo kwao hao Bombadier hivyo Tundu Lissu anaposema ndege imekamatwa siyo kweli.

“Hao watu hao wanaotudai wameenda kufile kesi ya kuzuia mali za Tanzania zisiondoke na serikali inaweza kutoa utetezi wake kwa hiyo hili suala ni kama linawekwa udalali na yote yanafanyika kutokana na umakini wa serikali ya awamu ya tano kwa hiyo wapinzani wanatafuta kiki tu” alisisitiza Msukuma

Siku ya Jumamosi serikali ilikiri wazi kuwa ni kweli kuna mgogoro uliopelekea ndege hiyo kushindwa kuingia nchini Tanzania mwezi Julai kama ambavyo ilitangazwa awali na kusema serikali imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *