Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma amefunguka na kumtuhumu RPC mkoa wa Geita na kusema ana roho mbaya kwani hajamtendea haki katika kumkamata licha ya kuwa kweli kulikuwa na makosa.

Msukuma amesema kuwa siku ambayo alikamatwa na kuwekwa ndani RPC huyo aliagiza chakula chake alicholetewa kimwage na kutaka Mbunge huyo ale chakula ambacho kinapatikana kituoni hapo jambo ambalo anasema alikataa na kulala na nja kwa sababu ya RPC huyo wa Geita.

Aidha Msukuma aliendelea kumtuhumu RPC huyo wa Geita kwa kusema kuwa wazungu wamemuwekea mafuta kwenye magari kuwatafuta madiwani wa CCM hivyo anahangaika na kutafuta madiwani badala ya kutafuta majambazi na watu wanaofanya uhalifu.

Msukuma amesema kuwa “Wazungu wamemuwekea RPC mafuta kwenye magari kusaka madiwani badala ya kumuwekea mafuta kusaka majambazi, kule nimekutana na askari wengine wana roho nzuri wanakuhudumia vizuri yaani unaona kabisaa upo sehemu ya usalama, lakini sijawahi kuona mtu ana roho mbaya kama huyu RPC wa mkoa wa Geita”.

Mbali na hilo Msukuma amempa siku tatu RPC wa Mkoa wa Geita awe amemuomba radhi kupitia kwa wazee wa mkoa huo kwa mambo ambayo ametendea na kusema kama hatafanya hivyo basi yeye ataanika mambo ya RPC huyo hadharani ili wananchi na Watanzania wote wajue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *