Bendi kongwe nchini, Msondo Ngoma inatarajia kufanya onesho maalumu la kufunga mwaka litakalofanyika Desemba 2 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya onesho hilo, Abdulfareed Hussein amesema onesho hilo litafahamika kama Family Day ambalo kwa mwaka huu ndilo litakafunga mwaka.

Fareed amesema kuwa burudani hiyo pia itaambatana na utambulisho wa baadhi ya nyimbo mpya zilizotungwa na wanamuziki wa bendi hiyo.

Amesema utambulisho wa nyimbo hizo utakwenda sambamba na kutambulishwa kwa wadau wapya wa bendi hiyo kongwe, wakiwemo wanamuziki mahiri.

Amesema Fareed kuwa, kutokana na unyeti wa utambulisho huo, jina la mwanamuziki huyo litabakia kuwa siri hadi siku hiyo ya onesho ndani ya ukumbi huo.

Ameongeza kuwa pamoja na hayo, pia burudani za siku hiyo zitalingana na ukweli kuwa, onesho hilo ndilo litakalofunga mwaka 2016, kisha utaratibu utaelekezwa kwa mwaka ujao wa 2017 baada ya kufanyika tathmini mbalimbali za maonesho yaliyopita.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *