Aliyekuwa msimamizi msaidizi wa wa tume huru ya uchaguzi IEBC katika uchaguzi mkuu nchini Kenya Kaunti ya Siaya, Caroline Odinga amekutwa amefariki dunia huku Jeshi la Polisi likisema kuwa upelelezi unafanyika wa kubaini wahusika wa tukio hilo.

Mwili wa mwanamke huyo ulikutwa katika soko la Sega Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando katika kijiji cha Lifunga.

Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema kuwa uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kujeruhiwa vibaya.

Hata hivyo, Familia ya marehemu huyo imesema kuwa mara ya mwisho marehemu alitoka nyumbani akielekea kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi katika Uchaguzi Mkuu ulioisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *