Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa katika Bunge lijalo linatarajiwa kuanza Novemba 7 mwaka huu anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue.

“Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba”.

Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *