Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa amemtaka Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ kuacha kulalamika na atulie ili polisi wafanye kazi yao.

Ameyasema hayo mara baada ya Mbunge Musukuma kumlalamikia RPC wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo kuwa ana roho mbaya na hakutumia busara kumkamata.

Amesema kuwa Musukuma anapaswa kutulia na kukaa kimya ili jeshi la polisi lifanye kazi yake kwani yeye ni mwananchi kama walivyo wengine wanaochukuliwa hatua hivyo hatakiwi kulalamika.

Amesema kuwa “Msukuma povu la nini, waache polisi wafanye kazi yao, kwani wewe ni mwananchi kama wengine, hivyo punguza kulalamika,acha haki itendeke,”.

Musukuma alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Geita na kulala rumande kwa muda wa masaa 24 kwa kosa la kuhamasisha maandamano yaliyopelekea kufungwa kwa barabara inayoelekea katika mgodi wa GGM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *