Msichana wa miaka saba amuandikia barua Donald Trump

0
366

Msichana wa miaka saba kutoka Aleppo ambaye kwasasa anaishi nchini Uturuki, Bana Alabed amemuandikia barua ya wazi Rais mpya wa Marekani, Donald Trump akimtaka kuchukua hatua kuhusu watoto wa Syria.

Katika barua yake hiyo kwa Trump msichana huyo ameandika “Lazima uchukue hatua kuhusu watoto wa Syria kwani ni sawa na watoto wako mwenyewe na wanahitaji amani kama wewe mwenyewe,”.

Bana alifanikiwa kuondoka Aleppo pamoja na familia yake Desemba mwaka jana wakati wa mpango mkubwa wa kuwaondoa raia maeneo yaliyodhibitiwa na waasi nchini Syria.

Ukurasa wake wa Twitter ulipata umaarufu kutokana na ujumbe alioandika akiwa maeneo ya mashariki mwa Aleppo wakati maeneo hayo yalikuwa yamezingirwa na wanajeshi wa serikali.

Mama yake mzazi amesema kuwa Bana aliandika barua hiyo siku kadha kabla ya Trump kuapishwa kuwa rais, kwa sababu alikuwa anamuona Trump mara nyingi kwenye runinga.

LEAVE A REPLY