Muongozaji filamu raia wa Iran, Asghar Farhadi amemkosoa rais wa Marekani Donald Trump na kumtaja kuwa mkosa utu baada ya filamu yake ya The Salesman kushinda tuzo la filamu bora ya lugha ya kigeni katika tuzo za Oscar.

Farhai alisusia sherehe lakini aliwakilishwa na watu wawili wenye uraia wa Iran na wenye asili ya Marekani.

Mahakama za Marekani zilizuia marufuku ya kusafiri lakini uongozi wa Trump tena unaandaa amri nyingine kuu.

Marufuku ya awalia iliwazuia kwa muda wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi duniani.

Mmoja wa wale walioteuliwa kumuakilisha Farhadi ni mhandisi mzaliwa wa Iran ambaye sasa ni mwanasayansi mmarekani wa anga za juu Anousheh Ansari, ambaye alisoma hotuba yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *