Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.

Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Walinzi wake wawili ambao alikuwa nao ndani ya gari hilo pia walioandamana naye pia wameuawa.

Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.

Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake.

Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho wakimsubili kwa ajili ya mkutano huo.

Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *