Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Shawn Spicer, amejiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kupinga mabadiliko ya Timu ya Mawasiliano ya Ikulu hiyo.

Bw. Spicer ameachia wadhifa huo, kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa kumteua, Anthony Scaramucci kuwa Mkrugenzi mpya wa Mawasiliano wa Ikulu.

Mabadiliko hayo yanafanyika wakati White House ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka jana.

Gazeti la New York Times linaarifu kwamba, Bw. Spicer alipinga vikali uteuzi wa Bw. Scaramucci kama Mkurugenzi wa Mawasiliano akidai ni kosa kubwa.

Bw. Scaramucci, ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mike Dubke kujiuzulu Mei mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *