Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami kusema kuwa alitongozwa na muigizaji Irene Uwoya, msanii huyo amejishusha na kumuomba radhi muigizaji huyo kwa kauli hiyo ambayo aliitoa hadharani.

Msami amesema kuwa haitaji kuwa na uadui na muigizaji huyo kwani licha ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na kutengana, lakini bado wanasaidiana na Uwoya ni mtu muhimu kwenye maisha yake.

Msami amesema kuwa “Irene ni mshikaji wangu sana. Hata baada ya kuachana bado tunasaidiana sana.

Mimi sipendi unapotengana na mtu halafu ukaanza kuonyesha kwa watu kuwa tumeachana haijengi picha nzuri kwani huzaa chuki. Kwa kauli yangu niliyoitoa kama nilimkwaza mtu nakiri kwamba naomba msamaha.

Pamoja na hayo Msami ameongeza kuwa “Nataka kutengeneza fan base yangu napenda mashabiki wa Uwoya waendelee kunisapoti muziki wangu na mimi mashabiki zangu waendelee kushabikia kazi za uwoya na siyo chuki.

Baada ya Msami amesema kuwa ametukana sana kwenye mitandao kutokana na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Irene Uwoya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *