Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami amemjia juu AT na kumtaka aboreshe kazi zake badala ya kulalamika kuwa kuna watu wanaobebwa.

Kutokana na hayo msami amemuonya kwamba wasanii anaowaita wacheza shoo wana maisha mazuri na mafanikio makubwa kumzidi yeye anayeimba.

Msami ameonesha kukerwa na kauli ya AT iliyodai kuwa wanaobebwa kwenye muziki ni wale wanao ‘dance’ huku wakiwa hawajui kuimba.

 

Katika hatua nyingine msanii huyo ameongeza kwamba AT hana ubora wowote kikazi ndiyo maana hawezi kuleta changamoto na wala hajawai kufikiria kufanya naye kazi, huku akimkumbusha kuwa hao anaowaita wacheza show huwa anawatafuta kipindi anapokuwa anawahitaji kikazi. 

 

 

Pia ameongeza kwa kuwataja wasanii kutoka kundi la Makomando kwamba ni wabunifu lakini wakati huo huo wana uwezo mkubwa wa kuimba kuliko AT hivyo inampasa kuwaheshimu hao anawaita ma -‘dancers’ kwa sababu Mungu pekee ndiye ameamua wafike walipofikia.

 

Msami ameongeza kwa kusema kuwa yeye kabla ya kuanza kuimba alikuwa mcheza show na mafanikio makubwa aliyapata kupitia kazi hiyo kama kununua gari lake la kwanza, kujenga nyumba na kuhudumia familia yake hivyo kumtaka AT asizungumze mambo asiyoyajua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *