Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi amesema masuala yote ya siasa yanayoendelea miongoni mwa vyama hapa nchini yatatuliwa katika meza ya majadiliano na si vinginevyo.

Jaji Mutungi amesema kuwa kunataharuki na hofu ambapo inajengwa kwa wadau wa siasa nchini ambapo inahitaji kuwepo kwa mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.

Msajili huyo amesema utawala bora ni kuheshimu miondomindu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundomindu itakuwa haijatendewa haki nchini.

Jaji Mutungi ameendelea kwa kusema kwamba Baraza la vyma vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbali mbali ya siasa ambayo yamejitokeza hivi karibuni.

Pia msajili huyo amesema siku zote watu wanatafuta muafaka wa jambo lolote katika meza ya mazungumzo ili kupata suluhu na kulinda amani ya nchi iliyopo sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *