Kesi inayomkabili meneja wa Diamond pamoja na Tip Top Connection, Babu Tale imeibua sura mpya baada ya msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza kujitoa kusikiliza shauri la kesi hiyo.

Kahyoza amefikia uamuzi huo juzi siku aliyopanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao.

Hatua hiyo inakuja baada ya mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde kumuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.

Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama hiyo.

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilimtaka Babu Tale amlipe Shekh Hamis Mbonde, shilingi milioni 250 kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila idhini ya Shekh huyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *