Mfalme wa Singeli nchini, Msaga Suma amefunguka mafanikio na changamoto alizopata baada ya kuachia wimbo wake wa Mwanaume Mashine.

Msaga Sumu amesema kuwa amepa muitikio mkubwa mtaani kutokana na ujumbe wake kwenye wimbo huo aliouchia mwezi Mei mwaka huu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa wimbo huo umekuwa na mafanikio makubwa ila mashabiki wamekuwa na tafsiri ambayo siyo.

Msaga Sumu amesema kuwa “Mashabiki walivyopokea wamepokea kitofauti ndio sababu ya kupendwa, mashabiki wamepokea kama nimeenda kinyume fulani, wanavyoona kama nimeleta matusi fulani ndio maana ilipokelewa kwa ghafla na haraka,”.

Pia amesema kuwa “Sisi watu wa uswahilini tuna maneno yetu na nilijua nikitoa nyimbo hii watu wengi watajua nimeenda kinyume lakini kumbe mimi nipo sahihi,”.

Msaga Sumu ameeleza kitu alichokusudia katika ngoma hiyo siyo ambacho watu wanahisi kwani amelenga kumsifia Mwanaume kuwa ni mpambanaji na mtafutaji na anaongoza familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *