Mwanamuziki wa Singeli nchini, Msaga Sumu amesema kuwa nyimbo mpya inayofanya vizuri kwasasa ‘ Iga Tena’ siyo dongo kwa mtu yeyote bali ni ujumbe kwa jamii nzima ya watanzania.

Msaga Sumu ameongeza kwa kusema kuwa huo ni ujumbe kwa watu wote ambao wamekuwa na kawaida ya kukopi vitu vya watu bila kuumiza vichwa wala kutambua kazi ya muanzilishi.

Mkali huyo wa Uswazi amesema ameamua kuwa serious katika muziki huo na ndiyo maana amefanya kitu kikubwa zaidi katika video ya wimbo wake huo mpya ambapo ameonesha mazingira halisi ya uswahilini.

Msaga Sumu amesisitiza kuwa yeye ndiye baba wa muziki wa singeli na hakuna mtu atakayeweza kumfunika kwasasa kutokana na kuutoa mbali muziki huo.

Amesema ameitoa mbali singeli tangu enzi za vigodoro kiasi cha kutishiwa kupelekwa mahakamani na baadhi ya wasanii wa taarab, kwa madai kuwa alikuwa akitumia muziki wao na kuingiza sauti yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *