Msafara wa bondia Floyd Mayweather, umeshambuliwa kwa risasi na watu wasio fahamika jumanne hii,huko Atlanta, Marekani,na kupeleke mmoja kati ya walinzi wa bondia huyo, Gregory La Rosa kujeruhiwa mguuni.

 

Polisi mjini Atlanta, wamethibisha kuwa Mayweather alikuwemo kwenye moja ya magari matatu wakati gari moja wapo liliposhambuliwa kwa risasi na kuhama njia huku watuhumuwa wa tukio hilo wakifanikiwa kutoroka.

 

Aidha,inaelezwa kuwa Mayweather alikuwa akistarehe kwenye klabu ya usiku kabla ya kuondoka na timu yake kurudi hotelini.Hata hivyo, haijafamiaka kama alikuwa akiviziwa na waharifu hao.

 

Wakati huo huo ,Mlinzi La Rosa, alikimbizwa hospitali baada ya kupata jeraha katika mguu wake na kasha kuruhusiwa muda mfupi baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *