Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Susan Kolimba amepokea msada wa chakula kutoka kwa waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana.

Msaada huo uliotolewa na waziri huyo wa Burundi ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera.

Msaada huo ni pamoja na mchele tani 100, sukari tani 30 mahindi tani 50 na majani ya chai tani 3.

Baada ya kupokea msaada huo, naibu waziri Kolimba aliishukuru Serikali ya Burundi kwa msaada huo uliotolewa kwa ajili ya wakazi hao wa Kagera ambao wamekumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha kupoteza makazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *