Staa wa Bongo fleva, Ali Kiba ametoa mchango wa milioni 21 kwa GSM Foundation kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo za kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Staa huyo amesema ameguswa na tatizo hilo ambalo limekuwa likiwasababishia watoto ulemavu wa kudumu pamoja na vifo.

Pia Kiba amesema ameguswa na kampeni ya GSM Foundationt katika kuwasaidia watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Staa huyo aliongeza kwa kusema toka taasisi hiyo wameanza shughuli ya kutoa huduma hiyo mamia ya watoto wameokolewa kutokana na taabu walizokuwa wanazipata.

GSM Foundation wametoa ujumbe wa shukrani kwa Alikiba kwa kuguswa na jitihada za taasisi hiyo za kusaidia watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Alikiba ametoa mchango huo siku chake toka muimbaji mwenzake katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva, Diamond Platnum kutoa milioni 20 kwa taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya watoto hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *