Kiungo wa zamani wa timu ya Taifa Stars, Mrisho Ngassa anatarajia kuanza kuitumikia klabu yake mpya ya Mbeya City baada ya hati ya uhamisho (ITC) kukamilika.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda baada ya kuthibitisha kutua kwa ITC hiyo kutoka shirikisho la soka la Oman katika ya Fanja aliyokuwa anachezea kiungo huyo.

 

Mwenyekiti huyo amesema kuchelewa kufika kwa ITC hiyo hakukuwa na msuguano wowote baina ya vilabu hivi viwili kilichokuwa kinatokea  ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi  kwenye ofisi kulingana  na taratibu za nchi hizi mbili.

 

Ngassa amejiunga klabu ya Mbeya City akitokea Fanja FC ya nchini Oman ambnako hajadumu hadi nusu msimu kutokana na timu hiyo kutokuwa na mahitaji ya huduma yake kwasasa.

 

Kiungo huyi uhenda akaanza kucheza kwenye mechi ya ligi kuu kati ya Mbeya City na Mbao Fc siku ya Jumamosi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *