Mwanamuziki wa nyimbo za utamaduni nchini, Mrisho Mpoto ameendelea kupata shavu katika hafla mbalimbali zinazofanyika Ikulu baada ya kutoa burudani kwenye dhifa aliyoandaliwa rasi wa Zambia Edgar Lungu.

Katika hafla hiyo, msanii huyo ambaye sasa anatamba na wimbo wake ‘Sizonje’ aliimba wimbo unaosifu na kuelezea ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Zambia.

Wageni waalikwa walifurahia maneno yaliyomo katika wimbo huo, yakiwemo yale yaliyowaelezea waasisi wa mataifa hayo mawili, Julius Nyerere (Tanzania sasa ni marehemu) na Kenneth Kaunda wa Zambia.

Pia ameelezea kuhusu Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), bomba la mafuta la Tazama, na mambo mengine mengi, ambayo yanaunganisha nchi hizi mbili.

Hiyo si mara ya kwanza kwa Mrisho Mpoto kutoa burudani kwani alitoa buradani katika dhifa iliyoandaliwa alipokuja Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *