Mwanamuziki wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto ametumia akaunti yake ya Instagram kuwataka wananchi kuacha kumuandama mkuu mkoa, Paul Makonda kuhusu kufoji vyeti vya elimu.

Hayo yamejili kufuatia tabia ya baadhi ya wananchi kumuandama vibaya mkuu wa koa huyo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutumia vyeti feki vya elimu.

Kupitia ukurasa wa Instagram β€œHii nchi ya ajabu sana ukifanya vizuri lazima upate maadui mpaka wakushushe, ndiyo waanze kumpansisha mwingine. Wako wapi waliosema Makonda songa mbele usirudi nyuma? mko wapi mliomuita Makonda shujaa mkombozi wa Wa watoto wetu, leo kila mtu anamruka na kuona hakuna alichofanya This is not Fair at all,”.

Mpoto ameongeza kwa kusema β€œAngalieni utendaji wake Wa kazi na siyo vyeti vyake guys!! Songa Songa Songa Makonda kama ulivyosema hii vita siyo ndogo na ina wanafiki wengi. @paulmakonda @paulmakonda unawaona waleeeeeee ndiyo siyo watu wazuri kabisa!!,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *