Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini ameuawa na mwili wake kuchomwa moto baada ya kupotea siku kadhaa nchini humo.

Taarifa za kuuawa kwake zimetolewa na baba yake mzazi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Kwenye akaunti hiyo Baba mzazi wa marehemu amesema kuwa mwanaye amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umechomwa moto na kwamba muuaji wa tukio hilo bado anasakwa na polisi.

Kupitia akaunti yake hiyo ameandika “The boyfriend has confession, He killed and burned my daughter,”.

Habari za kupotea kwa binti huyo zilianza kusambaa mitandaoni kuwa anatafutwa kutokana na kupotea kwake tangu April 28 mwaka huu.

Rafiki wa karibu  wa marehemu Stephanie Leong aliandika ujumbe Facebook kiomba msaada kwa watu mbali mbali waliomuona rafiki yake huyo wampatie taarifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *