Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustine Mrema ameshauri waathirika wa dawa za kulevya kupelekwa hospitalini kupata tiba badala ya polisi kuwakamata na kuwapeleka mahabusu au gerezani ambapo huko hujazana bila kupata msaada wowote.

Mrema amesema atamwomba Rais John Pombe Magufuli kumrejesha kazini Mwalimu wa Sekondari, Emmanuel Roman ambaye alifukuzwa kwa ajili ya utumiaji wa dawa hizo, lakini hivi sasa ameacha baada ya kupata tiba na ushauri nasaha.

Mrema alitoa ushauri huo alipokutana na waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo amesema anapopelekwa gerezani mtumiaji wa dawa za kulevya atakuwa hajasaidiwa, kwani atazidi kuharibikiwa badala ya kurekebishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *