Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye pia ni Mwenyekiti wa wa chama cha TLP,  Augustino Mrema amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akubali kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na akae kimya hadi mwaka 2020.

Mrema amesema hayo Jijini Dar es Salaam na kusisitiza kwamba alimtaka Waziri Mkuu Mstaafu watoke CCM pamoja kwa kuwa nguvu ya upinzani ilikuwa kubwa sana.

mrema1bc
Mrema aliongeza kwa kusema kwamba Chama cha Mapinduzi kilitakiwa kuondoka madarakani mwaka 1995 ambapo yeye ndiye alikuwa na nguvu kubwa ya kisiasa nchini.

Aidha Mrema amewataka vijana kuwa makini na upinzania kwa kuwa Lowassa alijiunga na upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea Urais ndani ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano kwani hayana faida kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *