Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema kuwa ofisi yake imeandaa mradi utakaonufaisha shule za msingi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

January amesema moja ya changamoto za Wilaya ya Bagamoyo ni ukame unaotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, uliosababisha kupanda kwa kina cha bahari na kusababisha visima vilivyochimbwa pembeni mwa miji na fukwe za bahari kufukiwa na maji na chumvi.

Ofisi ya Makamu ya Rais imeamua kuisaidia Wilaya ya Bagamoyo kuchimba visima kumi na saba virefu kwenye maeneo ambayo yameathirika na kupanda kwa kina cha maji na maeneo yenye ukame mkubwa,”.

Takribani kila kisima kitagharimu Sh milioni 50 na Ofisi ya Makamu wa Rais pia itaandaa mfumo wa kuvuna maji katika shule tano mradi utakao gharimu takribani Sh milioni 170.

Katika hatua nyingine, alitembelea Kiwanda cha Sea Salt kilichopo Saadani kuona namna kiwanda kinavyofanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *