Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Mr T Touch amefunguka na kusema kuwa yeye sio mtu wa kiki kwa hiyo kinachoondelea yeye na Chid Benz ni kweli.

Kupitia akauni yake ya Instagram ameandika kama ifuatavyo. Sio Kila Anayefanya Sanaa ni Mtu Wa Kiki,Sijawahi Kufanya Kiki Toka Naanza Muziki Mpaka Leo.

Bali Nilichokifanya ni kwaajili ya Usalama wangu na Hata wakwake Yeye Chid benz,Kwasababu Sidhani Kama Ningeamua Kushindananae Kwa Kupigana Ningemshindwa Kumpiga Sio Kweli.

Ila Ingetokea yeye kudhuhurika au mimi Nigedhuhurika Tusingekuwa Tunaongea haya Sahivi,Ndomaana Kabla Sijapost insta Nilienda police Kwanza Kuchukua RB Ili Sheria ifwate Mkondo.

Mimi Sio Muoga Wala Sio Mnyonge,Chid Haniwezi kwa Lolote Lile Lakini Nimeamua tuu Kufwata Sheria Bila Kutafutana Mitaani.

Halafu Kitu Kingine Mnaoongelea Swala La Mimi Kupost Insta Kama ni Kosa Ingetokea Labda Mimi Nimeuwawa picha Zangu Msingeziona Insta? kwasababu Chid alinifwata akiwa Ameshika Chupa Ambayo Imvunjwa Mkononi Je Nisingeweza Kujiokoa Kwa Kutumia Nguvu Ingekuwaje?.

Halafu Kitu Kingine Chid ni Maarufu na Mimi Pia Ni Mashughuli Kwa hiyo Sijaona Kama Kuna Ubaya Juu Ya Mimi Kuandika Insta Ili Watu wajue Kinachoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *