Mwanamuziki aliyekuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye amesaini mkataba na kampuni ya usambazaji wa muziki kutoka nchini Marekani inayoitwa kwa jina la ‘Empire’.

Peter Okoye ambaye jina lake la kisanii anatumia Mr P ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram huku akiweka picha akisaini.

Msanii huyo ameonyesha kufurahia hatua hiyo kwa kuandika kwenye mtandao wake wa Instagram, “Thank you Lord??? RepostBy @empire: “Just had a digital distribution deal with @peterpsquare! Welcome to the #EMPIRE family!” (via #WhizRepost @AppsKottage).”

Kampuni ya Empire ambayo makao yake makuu ni San Franciscomjini California, inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Kendrick Lamar pamoja na makampuni mengine makubwa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *