Staa mkongwe wa Bongo fleva, Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice ameelezea sababu zilizompeleka nchini Kenya kufanya ziara ya kimuziki.

Muimbaji huyo kwa sasa yupo nchini Kenya akifanya show kwenye maeneo tofauti ya nchi hiyo na kuitaja kampuni kutoka Nigeria ndiyo imempeleka nchini humo.

Mr. Nice amesema kwasasa yupo Kenya kuna kampuni ya Nigeria imempa dili la kufanya ziara katika maeneo tofauti nchini humo.

Mkongwe huyo  pia amesema ana project na wasanii wengine wa Kenya ambao wamemuomba afanye nao kazi, wasanii hao ni Jaguar na Wyre.

Mr. Nice amongeza kwa kusema kwamba mungu akipenda mambo yake yatakuwa mazuri kutokana na ziara hiyo kuona ina manufaa kwake kwasababu mashabiki wake wanamuonesha mapenzi za dhati.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *