Mwanamuziki wa Bongo fleva,  Mr Blue amedai kuwa watu wengi walikuwa wakitamani kuona collabo kati yake pamoja na Ali kiba jambo ambalo lilikuwa linawindwa kwa muda mrefu.

Mr Blue amesema kwamba watu wengi walikuwa wakimshauri yeye afanye kazi na Alikiba pia Kiba alikuwa anashauriwa na watu pia afanye kazi na Mr Blue.

Brue amesema ushirikiano wa kazi yake na Alikiba ulikuwa unawindwa kwa muda mrefu sana, watu wengi walikuwa wanaomba  afanye kazi na Alikiba na huku Alikiba nae walikuwa wakimwambia kama utafanya kazi na Mr Blue itakuwa kitu kizuri.

Ali Kiba
Ali Kiba

Brue ameseongeza kwa kusema kwamba anamshukuru Mungu kitu hicho kilifanyika na matokeo yake yameoneka kwani mbali na kupata pesa ambazo ameingiza kwa muda mfupi toka wimbo kutoka lakini wimbo huo umebahatika kuchezwa katika kituo kikubwa Afrika bila yeye kupeleka kazi hiyo.

Mbali na hilo Mr Blue amedai kuwa mafanikio mengine katika wimbo huo ni pamoja na kuwa na ‘viewers’ zaidi ya milioni moja ‘Youtube’ hivyo imekuwa ni video ya kwanza ya Hip hop kutoka Tanzania kufikisha watazamaji wengi ‘Youtube’.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *