Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Mr Blue amefunguka na kusema kuwa yeye alianza muziki kwa kuiba ‘verse’ ya mtu kipindi alichokuwa mdogo.

Mr Brue amesema kuwa wakati alivyoiba hizo verse na kuanza kuimba na alipata shangwe sana kwa watu ndiyo kitu kilichomsukuma kufanya muziki.

Pia Mr Blue amedai kuwa yeye alikuwa anaishi Kariakoo lakini nyumbani kwao kulitokea matatizo ya kifamilia hivyo alihama na kwenda kukaa Tandale na huko ndiko anadai kulikuwa chimbuko lake la muziki kwani watu aliowakuta huko walikuwa wanafanya muziki.

Mr Blue amesema kuwa “Kwa hiyo nilipohamia huko ndiko kulikuwa nyumba ya muziki, nikajikuta nawasikiliza sana na kukariri ‘verse’ hivyo kuna siku nilikwenda sehemu na kuchana verse ya mtu nilishangiliwa sana, kwa hiyo mimi naweza kusema nimeingia kwenye muziki kwa kuiba ‘verse’ ya mtu ambaye naye nilimkuta huko nilikohamia”.

Aidha Mr Blue amesema kuwa katika maisha yake ya muziki amekosa mengi ambayo alikuwa anastahili kuyapata kwenye muziki wake kama tuzo mbalimbali na jasho lake kwenye album zake alizotoa kipindi cha nyuma kwani hakunufaika nazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *