Mwanamuziki wa Muziki wa Asili nchini, Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amesema kuwa amefurahishwa na kauli ya China ya kutaka kukomesha biashara ya meno ya tembo nchini.

Hayo ameyasema jana wakati wa matembezi ya amani yaliyoandaliwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing ambaye alisema kuwa nchi yake iko kwenye mkakati wa kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu biashara hiyo itakuwa imeishakufa kabisa.

Mpoto alipopewa nafasi ya kuzungumza kuhusu hatua ya China alisema kuwa ni hatua nzuri na itasaidia katika kupambana na kutokomeza ujangili wa meno ya tembo nchini.

Hata hivyo Mpoto aliongezea kuwa suala la kupinga ujangili nchini siyo la mtu mmoja, kila Mtanzania ana haki ya kulinda maliasili za nchi yake kwa ajili ya kizazi kijacho, na hivi karibuni anatarajia kuanzisha kampeni mbalimbali ambazo zitawafanya Watanzania kufichua majangili kwa kuwa ni watu ambao wanatoka katika jamii zao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *