Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amesema mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli si waoga na wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais katika masuala mbalimbali.

Mpina aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu huku akisikitika kuwa maneno yanayotolewa dhidi ya mawaziri na manaibu na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wao ni waoga na hawamshauri Rais si sahihi.

Amesema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakibeza utendaji wa Baraza la Mawaziri na kuwaita waoga wasiomshauri Rais.

Katika kudhihirisha kuwa wanatekeleza wajibu na kumshauri Rais, Mpina alisema Serikali iliamua kumnyang’anya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye shamba la hekta 33 kwa kushindwa kuliendeleza.

Amesema wataendelea kuchukua hatua bila ubaguzi wa aina yoyote kwa wasiotaka kufanya kazi kwa kufuata utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *