Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri mbali mbali hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema kwamba ni vyema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Majaliwa amewataka watendaji hao wa Halmashauri kuwa makini na matumizi ya fedha hizo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea zitamuunguza.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo jana  wakati akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Azimio Wilayani Mpanda.

Pia Waziri Mkuu aliongeza kwa kusema ni lazima wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *