Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho huenda akakumbwa na adhabu kutoka Chama cha Soka Uingereza (FA) baada ya kufukuzwa uwanjani na refa kwenye mechi dhidi ya West Ham.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mourinho alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada ya kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.

Vile vile Mourinho aliwahi kufukuzwa uwanjani mwezi uliopita na refa Mark Clattenburg wakati wa mechi iliyomalizika sare 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Burnley.

Refa Moss pia aliwahi kumfukuza uwanjani Mourinho Oktoba 2015alipokuwa anaikufundisha kikosi cha Chelsea wakati wa mechi dhidi ya West Ham.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *