Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema haamini kwamba atastaafu ukocha akiwa bado katika klabu hiyo ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

Mreno huyo wa miaka 54 ambaye kwa sasa anahudumu kwa msimu wake wa pili kama mkufunzi Old Trafford hajawahi kukaa zaidi ya miaka minne katika klabu moja.

Akiongea na runinga moja ya Ufaransa, Mourinho alisema anafikiri kwamba Paris St-Germain ni klabu nzuri sana.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Porto aliambia kipindi cha Telefoot cha TF1 kwamba: “Siamini, hapana, sina uhakika kwamba nitafikisha kikomo ukufunzi wangu hapa.”

Alipoulizwa iwapo alikuwa anamaanisha IManchester United, Mourinho alisema: “Ndio”.

Mourinho, aliyeshinda Kombe la EFL na Europa League msimu wake wa kwanza Old Trafford, amesema mtoto wake wa kiume amekuwa akitazama mechi za PSG sana karibuni.

Mkataba wa Mourinho kwa sasa ni wa miaka mitatu na anaweza kuongezewa mkataba huo hivyo basi anaweza kusalia United hadi 2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *