Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameiambia klabu ya Real Madrid kuwa wajipange kama wataka kumsajili kipa wake, David De Gea.

Mourinho amemtaka Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez, kuwa wakitaka kumsajiri De Gea inabidi wajipange kwa pesa ndefu.

Mourinho amesema kuwa “Real Madrid wanapaswa kujipanga kuhusu usajili wa mlinda mlango huyo, na kama watakaa hovyo, huenda wasimpate kirahisi kama wanavyofikiia”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Mlinda mlango huyo ana thamani kubwa na ikitokea Manchester Utd inaridhika na kiasi cha pesa watakacho kitangaza kama ada yake ya usajili, hatokua na hiyana kumruhusu De Gea kuondoka.

Mwanzoni mwa msimu wa 2015/16, De Gea alikaribia kuondoka Man Utd baada ya kuhusishwa kwa kipindi kirefu na taarifa za kurejea mjini Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *